Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Naibu Waziri Mhe.Jafo Afungua Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Mjini Dodoma

Naibu Waziri-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akizungumza na Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Manispaa,Majiji na Halmshauri wakati akifungua mafunzo ya siku tano yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi leo Mjini Dodoma.

Mtendaji MKuu wa Uongozi Institute Prof Joseph Semboja akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Uongozi kwa wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Manispaa,majiji na Halmshauri leo Mjini Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Hapi akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Manispaa,Majiji na Halmshauri katika ufunguzi wa Mafunzo ya siku tano yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi leo Mjini Dodoma.

Baadhi ya Wakurugenzi wa Manispaa,Majiji na Halmshauri wanaohudhuria mafunzo ya Uongozi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi wakisikiliza mada mbalimbali katika mafunzo hayo leo Mjini Dodoma.

Naibu Waziri-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akizungumza jambo na Naibu Katibu Mkuu-TAMISEMI Mhe.Dkt Zainabu Chaula wakati wa mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Manispaa,Majiji na Halmshauri yanayofanyika Mjini Dodoma na kuendeshwa na Taasisi ya Uongozi.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Josephine Matiro na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe.Richard Kasesela wakimsikiliza Naibu Waziri-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo ya siku tano kwa wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Manispaa,Majiji na Halmshauri leo Mjini Dodoma. (Picha na: Daudi Manongi)

23 thoughts on “Naibu Waziri Mhe.Jafo Afungua Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Mjini Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *